
Gazeti
la DJ na: Gerald Joseph/DjGeric
Pesa ni kitu kilichopewa
thamani na kikapewa uwezo wa kutumika katika hali tofauti hasa ile hali ya
kubadilishana na vitu vingine yaani kununua au kuuza vitu. Ila sasa…
Pesa
hii ambayo ipo katika muundo wa noti na sarafu sio marighafi ya kuzalisha hivyo
vitu vingine ambavyo inabadilishana navyo, mfano magari, vyakula, nguo, mafuta
nakadhalika. Kiasi kwamba hata bila pesa vitu hivyo vingeweza kuwafikia watu
kama ilivyo sasa.
Mfano; wanaosafirisha
bidhaa kwenye vyombo mbalimbali hawatumii pesa kubeba hizo bidhaa, wanaozalisha
mafuta hawatumii pesa kutengeneza mafuta hayo au wanaotengeneza nguo hutumia
vitu vingine na sio pesa
UTAMU
WA PESA
Pesa imekuwa tamu kiasi
kwamba hata watu wameitukuza kuliko kitu kingine chochote. Imefika mahali watu
wanafanya mambo ya kuwateketeza ndugu na jamaa zao kwa sababu ya kuitafuta
pesa.
Pia imekuwa vigumu sana
kupata mahitaji ya kumwezesha mtu kuishi bila pesa, mambo kama chakula, mavazi
na malazi na hata vinginevyo. Lakini pia mambo ya starehe nayo bila pesa ni
vigumu sana kuhusika nayo zaidi ya kubaki kuyasikia tu masikioni mwa watu
wengine. Jambo linguine na nyeti sana ni swala la afya ambapo kuna hospitali
mtu hapati huduma kabla ya kuonesha kadi ya malipo hata kama ana hali gani,
hivi vyote na vingine ambavyo sijataja hapa ni kuonesha namna gani pesa
inapendwa na karibia kila mtu alihali pesa hii sio marighafi.
MAONI
YA MHARIRI
Lengo na dhumuni la
gazeti hili la dj sio kushusha thamani ya pesa ya nchi au mtu yeyote au
kuwasema waliotengeneza pesa bali ni kuonesha namna ilivyopewa sana kipaumbele
kuliko hata maisha ya mtu, kwa sababu wako watu ambao wanadiriki hata kuwaua
wazazi au watoto wao au mtu yeyoye ili wapate hio pesa ambayo sio marighafi.
Pia lengo la gazati
hili ni kuwahimiza watu au jamii kukemea njia zote mbaya zinazotumika kuitukuza
pesa kuliko uhai wa mtu.
Imetolewa Na,
Gerald Joseph/DjGeric
kwa
maoni tuandikie kutumia barua pepe: gericfm@gmail.com
PESA SIO MALIGHAFI!
Reviewed by GericFM
on
June 21, 2017
Rating:

No comments: