Geric FM

Gazeti la Dj

                                           GAZETI LA DJ 7th July 2017

UNDERGROUND habari imeandikwa na Juma kasanzu

Underground ni neno ambalo tumekua tukilisikia sana hasa katika tasinia ya burudani hapa tanzania (muziki) likimanisha msanii ambae  mchanga bado hana mashabiki wengi au hajatambulika sana

Lakini kwa maana hiyo neno hili pia tunaweza kulitumia katika hali nyingine na muhimu sana katika jamii mfano:
KIJANA anae anza maisha  nae kwa namna moja ama nyingine tunaweza kumwita kama underground (kiuchumi)  katika nchi zinazo endelea kama Tanzania huwa vijana tunaanza maisha katika hali ngumu kipesa . Hivyo basi vijana wengi tunajikuta tunaanza kutafuta maisha kwa kiasi kidogo sana cha pesa ambazo tunazipata kutokana na shughuli zetu ndogo ndogo tunazo  anza nazo katika safari yetu ya kimaisha  kisha kufikia kupata pesa nyingi na kuachana na uanderground wa kiuchumi kama ilivyo kwa hao wasanii wachanga wakishafanikiwa na kuwa Star.

Tukirudi katika upande wetu wa pili (katika uchumi) kijana pia usijisikie vibaya kuwa na kipato kidogo kaza kamba ya kujishughulisha wakati huo ukikimbilia Ustar kwa maana ya kipato kikubwa na kuachana na uanderground
MICHEZO habari imeendikwa na  A. Steve
Tiketi za kuhudhulia FIFA WORLD CUP 2018 wenyeji wake wakiwa Russia zitaanza kuuzwa baada ya tarehe 1 december 2017 mara baada ya mechi za kufuvu kuingia katika shindano la word cup tarehe 1 december.

SABASABA habari imeandikwa na Gerald Joseph
Leo ikiwa ni siku ya sabasaba sherehe ambayo inaedelea hapa tanzania hadi tarehe 13 mwezi huu, Gazeti la Dj linakukumbusha kuwa siku kama hii iliwahi kuwepo miaka ya nyuma ila katika siku tofauti kama ifuatavyo:
Mwaka 2014 ilikuwa J3, 2015 J4, 2016 Alhamisi na pia mwaka 2020 itakuwa siku ya J4.

MAONI YA MHARIRI
Leo gazeti la dj limekuaa na habari ndefu na nyingi hii ikiwa ni maboresho ya huduma zetu katika kutimiza nia na madhumuni ya GML, na hii imetokana na maoni ya wasomaji wa gazeti hili.



Kwa maoni na ushauri tuandikie kupitia: gericfm@gmail.com au WhatsApp namba: 0689492656


Limetolewa na DjGeric
@Geric Media Live (GML)
Gazeti la Dj Gazeti la Dj Reviewed by GericFM on July 08, 2017 Rating: 5

No comments:

Vistros

Powered by Blogger.