www.spreaker.com/gericfm
geric fm ni radio ya mtandaoni ambayo unaweza kuisikiliza kupitia http://www.spreaker.com/gericfm iliyoanzishwa na kijana (GERALD HALIUS JOSEPH) mwenye ndoto za kuwa mtangazaji wa radio na mwenye mapenzi na muziki. Hii ilitokana na yeye kuhitaji mahali pa kufanyia mazoezi na uzoefu wa kutangaza, kuandaa vipindi na kadhalika.
kabla ya kuanzisha Gericfm aliwahi kuwa na radio zingine mtandaoni kama vile kabox fm, Taranta fm na DjGeric FM zote hizi lilikuwa mtandaoni hadi pale muda ulipoisha kwa sababu hakuweza kulipia sever za hizo radio.
kutokana na changamoto mbalimbali anazopitia kijana huyu kutimiza ndoto zake ameona ni vizuri kuanzisha blog hii ili kutunza baadhi ya vipindi vya radio yake ili kuondoa tatizo la kupoteza kumbukumbu za kile alichowahi kukifanya na kuendelea kufanya.
OMBI LAKE KWAKO
wewe kama mmoja wa watu walioweza kuiona habari unaombwa kuisambaza ili aweze kujulikana na kupata watu wengi kumshauri na kusikiliza anachofanya kisha kufikia malengo yake.
pia kama kuna namna unaweza kumsaidia hata kupata baadhi ya vifaa kama vile microphones, mixer, speaker nk. atashukru sana. msaidie kuishi ndoto zake
imetolewa na
Gerald Joseph/DjGeric
mtangazaji wa radio/Dj
simu: 0743 536 577 na 0689 492 656
kuhusu Geric fm na Gerald
Reviewed by GericFM
on
May 20, 2017
Rating:
No comments: