GAZETI
LA DJ
ETI
KUJIONGEZA!
Katika maisha ya
wanadamu kumekuwa na ile hali ya kuboresha
maisha kwa kutafuta chakula, mavazi, nyumba nzuri, elimu na kadhalika. Lakini maisha
haya pamoja na hivyo vyote vinavyotafutwa vimetawaliwa sana na pesa.
Kwa maana kuwa bila
pesa inakuwa vigumu kuvipata vitu hivyo. Pia njia za kupata pesa zimekuwa
zikiwatatiza walio wengi sana na pia kumekuwa na wengi wanaoshauri au
kuhamasisha wenzao KUJIONGEZA.
Wakimanisha
kuwa watafute njia za kupata pesa ili kuweza kuyaboresha maisha yao, ni vizuri
sana kabisa kuelezana njia za kuishi vizuri ila tatizo ni pale wengi
walipolalia upande mmoja katika dhana hio ya kuiongeza, na upande huo ni wa biashara.
Hapa sio kila mtu
anawea kufanya biashara kama wanavyohamasisha baadhi ya watu. Na dhana hii ya
kufanya biashara inatokana na dhana nyingine ya ajira/kujiajiri.
Katika dhana hii ya
kujiajiri ni kwamba sio kila mtu pia anaweza kujiajiri licha ya kuwa na uwezo fulani
kama vile pesa na rasilimali zingine.
Hivyo kuwa na matabaka
ya wajiriwa na waajiri, nah ii ni kutokana na utofauti tulionao wanadamu katika
kuwaza na kuamua mambo katika maisha yetu.
Hivyo basi neon linalotumika
kwa kuwahimiza watu kutafuta njia za kupata pea na wengi wakimanisha kujiajiri
kuna watu linawafaa na kuna watu haliwafai wala kuwasadia kwa sababu kuna watu
wao wako hivyo yani aidha waajiriwe au watunzwe ili kuboresha maisha yao katika
kuhakikisha wanapata mahitaji muhimu na za ziada.
MAONI YA MHARIRI
Kabla ya kujiongeza
angalia uwezo wako katika swala zima la kuboresha maisha uliyonayo au kutimiza
mahitaji yako muhimu nay a ziada. Neno KUJIONGEZA lenye maana ya kujiajiri au
kufanya biashara kama wengi wanavyolitumia lisikufunge na kukufanya ukafanya
usiloweza eti kisa ndo wengi wanasema kinafaa.
Pia nia na lengo la
Gazeti la Dj sio kukinzana na wote wanahamashisha jitahada mbalimbali za
kuwaweza wengine kujikwamua na kuyaboresha maisha yao bali ni kuonesha utofauti
tulionao wanadamu pia kushauri zitafutwe mbinu zingine za kuwasaidia wasioweza
kujiongeza kwa kufanya biashara au kwa kujiajiri.
Imetolewa na kuandikwa na:
Gerald Joseph/DjGeric
WhatsApp namba: +255689 492 656
ETI KUJIONGEZA!
Reviewed by GericFM
on
June 06, 2017
Rating:

No comments: