Geric FM

MTU KATI

Gazeti la Dj.
MTU KATI na DjGeric
Imezoeleka kuwa watu hupenda kusaidiana katika mambo mbalimbali hasa watanzania. Sasa kuna wakati misaada inakuwa na migogoro ya nafsi, yani mtu anakuwa na maswali na majibu juu ya mwenzake bila kumwambia.

Leo hii ujua kuwa mfano mahindi yanauzwa shilingi mia tano, 500/= maeneo mengi hapa Tanzania, sasa utakapoamua kumuagiza mtu akusadie kukununulia na ukampa hio shilingi 500/= kuna haya yanaweza kutokea.

Akikuta mahindi yameshuka bei na yanauzwa shilingi mia nne 400/= akakuletea mhindi na shilingi mia moja 100/= kama chenji utajiuliza na kujijibu maswali yafuatayo:
            Je chenji imebaki hii kweli au nyingine amebaki nayo?
            Je amenunua kweli au wamemgawia na ameamua kula shilingi 400/= na kunipa hii mia moja?
            Au ananitega aone kama nitaichukua pesa yake bila sababu ya msingi na sio yangu?

Akienda akakuta mahindi yamepanda bei yanauzwa shilingi mia sita 600/=, akaamua kukununulia ili akija  umpe hio shilingi mia moja iliyoongezeka pia haya yatatokea:
           Mahindi yamepanda kweli au anataka kuniibia?
          akikupigia kukujuza kuwa mahindi yamepanda bei ili uamue kama anunue au aache?, 
          utadhani pia        hataki kukuletea ndio maana amekwambia bei kubwa ili useme asinunue.

mtu kati ina changamoto nyingi sana kama watu wasipokuwa makini katika kufikria. Ili kuepukana na migogoro ya nafsi kwa sababu ya mtu kati bora ufanye mwenyewe kama huwezi kuamini kuwa mambo hubadilika na pesa imetumika halali.

MAONI YA MHARIRI.
Gazeti la DJ halina maana kuwa tusisaidiane wala kuagizana vitu vinavyohusu pesa bali ni kuonesha  namna watu tunavyowaza na maisha halisi yalivyo katika baadhi ya mambo.

Imetolewa na:
Gerald Joseph/DjGeric

MTU KATI MTU KATI Reviewed by GericFM on June 04, 2017 Rating: 5

No comments:

Vistros

Powered by Blogger.