NGUVU
YA PAMOJA
Ule usemi wa umoja
ni nguvu umekuwa ukitumika katika mazingira tofauti ila kuna mahali
umesahaulika na hautiliwi maanani sana, ila leo naomba nikuoneshe namna
unavyoweza kujikumbausha na kuwakumbusha wengine.
Kuna watu wanataka kufanya mambo ambayo yanahitaji
pesa, ubunifu na usimamizi ila kwa bahati mbaya wanajikuta hawana vitu hivi
vyote kwa pamoja, kisha hutafuta watu wa kuungana nao ili kukamilisha mambo
hayo.
Ila sasa wale wenye pesa huona kama wao wanaweza
kufanya kila kitu kwa kuwa wana pesa wanasahau kuwa pia kuna ubunifu au
usimamizi wa jambo husika kisha hufanya na mambo huwa hayafikii malengo. Wanajiuiza
wapi kumekosewa na huishia kukosa majibu, kumbe wangeweza kutafuta washirika
katika jambo husika ingeweza kufanikisha jambo hilo.
Maana ambae hana pesa anaweza kuwa mbunifu au kuwa
msimamizi mzuri wa jambo husika. Sasa pesa, usimamizi mzuri na ubunifu
vikiungana lazima matokeo yawe mazuri.
MAONI
YA MHARIRI.
Lengo la gazeti la Dj ni kuonesha umuhiu wa watu
kuungana na kushirikiana katika baadhi ya mambo na kutatua changamoto kadhaa
zinazowazunguka kuliko kuwadhalau wasio na pesa na wenye pesa kujiona wanaweza
kila kitu.
IMETOLEWA
NA,
Gerald
Joseph/DjGeric
NGUVU YA PAMOJA
Reviewed by DjGeric
on
June 11, 2017
Rating:

No comments: