Geric FM

UWEZO WA SIMU YA MKONONI



Gazeti la DJ na Gerald Joseph/DjGeric
Ujio na matumizi ya simu za mkononi umekuwa msaada sana katika mambo mengi katika maisha ya wanadamu hasa hapa Tanzania.
 Msaada mkubwa wa simu umekuwa kama vile kutoa taarifa kwa haraka sana, kufanya vikao kupitia simu bila kusafiri, kutuma na kupokea pesa nakadhalika. Ila leo gazeti la Dj, limeandika juu ya mambo mawili katika matumizi ya simu za mkononi, nayo ni:


·         uandishi wa majina ya watu kwenye simu na
·         kuweka nywila (password)

UANDISHI WA MAJINA YA WATU KWENYE SIMU
Hapa ni kwamba watu wanatofautiana katika uandishi wa majina ya watu katika simu zao, kuna wanao andika kwa kutumia vifupisho, majina ya utani, majina halisi au kutumia uhusiano wa watu husika kama vile baba, mama, mjomba nakadhalika. Na kuna wanao andika majina ya ndugu kwa lugha ya kingereza mfano dady au mammy nakadhalika.

KUWEKA NYWILA (PASSWORD)
Pia hapa utakuta mtu anatumia simu yake lakini kila sehemu ameweka nywila (passwords) kwa maana watu wengine wasione au wasiweze kuona kilichopo au kutumia simu yake bila ruhusa yake. Na hii ni kwa zile simu za kisasa maarufu kama smart phone. Pia kuna ambao hawaweki hizo nywila.
Ndiyo kuna faida na hasara za kuweka nywila ila hasara ni kubwa kuliko faida.

FAIDA: mtu atakuwa huru kutumia simu yake atakavyo na kutunza siri ake nyingi katika simu yake.

HASARA: hapa ndo tunapoona jambo la msaada kutumia simu linashindikana kwa sababu ya nywila za simu hio. Mfano mtu anaishi nje ya familia yake alafu amepata shida labda kazimia au kaugua na hawezi kutoa taarifa hata mahali, kisha jirani au mtu anapita na kumkuta katika hali ngumu kama hio, kisha anamua kumsaidia kwa kutoa taarifa kwa ndugu au polisi au hosipitalini ili watoe smsaada lakini anashindwa kwa kuwa simu ya mgonjwa in nywila na aliekuja haijui.

MAONI YA MHARIRI
Kwa kuwa simu inaweza kuwa msaada mkubwa hasa wakati wa shida ni bora kuandika majina ya watu kwa usahihi yani bila kutumia vifupi, majina ya utani. Na kama ni uhusiano ni bora kuandika kabisa kama ni baba andika baba au mama au kaka, mjomba, nakadhalika.
Hii itasadia sana pindi mtu anapo patwa na shinda alafu hawezi kutumia simu ila watu walio karibu wanaweza kutumia simu yake na kutoa taarifa kwa ndugu ili kupata msaada zaidi au kutoa taarifa.
Pia kuhusu nywila ni bora simu akae bila nywila maana itakwambisha baadhi ya mambo hasa wakati wa shida.
Japo kuna wanaosema kuwa wanalinda pesa zao katika simu lakini pesa ina nywila zake katika simu kadi hivyo imelindwa tayari.

Imetolewa Na,
Gerald Joseph/DjGeric
www.spreaker.com/gericfm
UWEZO WA SIMU YA MKONONI UWEZO WA SIMU YA MKONONI Reviewed by GericFM on June 11, 2017 Rating: 5

1 comment:

  1. Enter your comment...safi Mzee nimekuelewa mnooooooo daaaaah

    ReplyDelete

Vistros

Powered by Blogger.